Habari

Imewekwa:: May, 04 2019
News Images

PAMBA KUNUNULIWA KWA TSHS 1,200/= MSIMU WA 2019-20

Msimu wa ununuzi wa pamba 2019-20 ulizinduliwa rasmi kitaifa mkoani wilaya ya Katavi mkoa wa Simiyu siku ya tarehe 2 Mei 2019 ambapo mkuu wa mkoa huo alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo. Jambo kubwa lilikuwa likisubiriwa na wakulima wengi ni kusikia bei ya pamba kwa msimuu huu itakuwa shilingi ngapi ambapo Mkuu wa Mkoa Ndg. Amos Makala alitegua kitendawili icho kwa kutangaza rasmi bei elekezi ya pamba mbegu kuwa ni TShs 1,200/= kwa kilo moja ya pamba mbegu.

Bei hiyo ni ongezeko la TShs 100 kutoka bei ya TShs 1,100/= ya msimu wa 2018-19. Mkoa wa Katavi ni moja ya mikoa iliyoanza kuibuka kwa kasi katika uzalishaji wa pamba huu ukiwa ni msimu wake wa pili tangu ilipoanza kulima msimu wa 2017-18 ambapo uzalishaji wake kwa msimu huu unatarajiwa kufikia tani 15,000 kutoka tani 500 msimu uliotangulia. Uzalishaji wa pamba kitaifa kwa msimu huu wa 2019-20 unatarajiwa kufikia tani 400,000 ambalo ni ongezeko la asilimia arobaini na tatu (43%) kutoka uzalishaji wa tani 230,000 msimu wa 2018-19.