Habari

Imewekwa:: Oct, 04 2021
News Images

Msimu wa ununuzi wa pamba 2021-22 umekamilika katika maeneo mengi nchini huku shauku ya wakulima wengi wakiwa na sahuku ya kutaka kulima zao ili msimu huu wa kilimo kutokana na mwenendo mzuri wa bei ya pamba ambapo katika baadhi ya maeneo ilifikia Tsh 1900 kutoka 1050 bei dira kwa kilo moja ya pamba iliyotangazwa msimu wa pamba ulipoanza

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Bw. Marco Mtunga alipofanya mahojiano maalum na chombo kimoja cha habari jijini Mwanza hivi karibuni. Bw.Mtunga amesema msimu huu wa kilimo wanatarajia wakulima wataitikia kwa wingi kulima zao ili kutokana na wakulima wengi kuhamasishwa na ongezeko kubwa la bei iliyochagizwa na uhitaji mkubwa wa malighafi hii kufuatia viwanda vingi duniani vya nguo vilivyokuwa vimefungwa kuanza kufunguliwa baada ya hatua ya upatikanaji wa chanjo ya gonjwa la Uviko-19

Dalili za kuongezeka kwa wakulima wa zao la pamba msimu wa 2021-22 linaisukuma Bodi ya Pamba kuandaa kiasi cha mbegu za kupanda cha kutosheleza mahitaji ya wakulima wote nchini ambapo kiasi cha tani 20,000 kimetengwa na baadhi ya maeneo wameshaanza kupokea mbegu kwa ajili ya msimu wa kilimo 2021-22

Mkurugenzi Mkuu amewaondoa hofu wakulima kwa kuwahakikishia kuwa hakuna mkulima atakayekuwa na nia ya dhati ya kulima akakosa mbegu sababu kiasi kilichotengwa ni kikubwa na mbegu za ziada tayari zimetengwa kama kiwango hicho hakitatosheleza.

Mbegu za kupanda zinazosambazwa zinazalishwa katika kiwanda cha kuchakata mbegu cha Jielong Holding Ltd cha mjini Shinyanga ambacho kina uwezo wa kuchakata tani 500 kwa siku na tangu uzalishaji uanze mwezi wa tisa matarajio kama alivyobainisha Bw. Mtunga ni kuwa hadi kufikia mwezi wa kumi na moja mwanzoni wakulima wote watakuwa wamepata mbegu zapamba.

Msimu wa kupanda pamba katika kanda ya magharibi inayozalisha 99% ya pamba yote kikalenda uanza tarehe 15 Novemba hadi 15 Desemba