Habari

Imewekwa:: Mar, 16 2022
News Images

TANZANIA KUANDAA MKUTANO WA NCHI WANACHAMA JUMUIYA YA PAMBA AFRIKA

 • Wadau mbalimbali kutoka mataifa ya Afrika yanayounda Jumuiya ya Pamba (ACA) wanatarajiwa kukutana jijini Mwanza-Tanzania kwenye mkutano wa 18 wa Jumuiya iyo unaolenga kujadili na kuweka mikakati ya kuleta maendeleo katika zao la pamba barani Afrika.

 • African Cotton Association (ACA) ni jumuiya inayounganisha mataifa na kampuni za Afrika zinazojishughulisha na pamba zikiwemo za binafsi na za Serikali.ACA ilianzishwa tarehe 19 Septemba, 2002 Cotonou nchini Benin. Dhumuni la kuanziswa ilikuwa ni kuwa na daraja litakalowaleta pamoja wadau wa pamba bara la Afrika ili kutetea maslahi mapana ya pamba katika bara la kimataifa.
 • Akizungumza na wanahabari jijini Mwanza, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) ambaye pia ni Rais wa Jumuiya ya Pamba Afrika anayemaliza muda wake,Ndg. Marco Mtunga amesema mkutano huo unatarajiwa kuanzia tarehe 17 hadi 18 Machi 2022 na kuhudhuriwa na makampuni mbalimbali ya ununuzi pamba duniani ukiwa na kauli mbiu Kauli mbiu ya mkutano ni “Tija na ubora ni muhimu katika kulifanya zao la pamba kuwa endelevu Afrika”.
 • .

  Mtunga ameeleza kuwa mbali na mkutano huo kuzungumzia maendeleo ya pamba barani afrika utawakutanisha wanunuzi wa pamba pamoja na wanaouza zao hilo kutoka mataifa mbalimbali.

  "Tanzania kama mwenyeji wa mkutano huo tutatoa taarifa yetu jinsi pamba inavyolimwa na kutunufaisha kiuchumi katika nchi ya Tanzania" alisema Mtunga.

  Naye Katibu Mkuu wa ACA kutoka nchini Mali, Fahala Adeyemi amesema nchi za Afrika Magharibi zimepiga hatua kwenye ulazishaji wa zao la pamba hivyo pamoja na mambo mengine mkutano huo utasaidia mataifa mengine ikiwemo Tanzania kubadilishana mbinu za kukuza uzalishaji wa zao hilo na kuwaimarisha kiuchumi wakulima.

  Kwa upande wake Balozi wa Pamba Tanzania, Aggrey Mwanri amesema jitihada mbalimbali ikiwemo utoaji elimu kwa wakulima namna ya kuandaa mashamba na kupanda mbegu kwa kuzingatia vipimo hatua itakayosaidia kuvuna mazao kwa tija hadi kufikia kilo 2,500 kwa hekari moja hatua ambayo tayari imefikiwa na mataifa ya Mali, Misri na Burkna Faso.

  "Wenzetu wa brazil, aljentina walifikia hatua hiyo na utafiti ukanonesha kuwa wamebadili vipimo" alisema Aggrey.
 • Wakati akimalizia Rais wa Jumuiya ya ACA ameongeza kuwa licha ya umuhimu mkubwa wa mkutano huu kwa wadau wa pamba nchini na barani Afrika lakini vilevile mkutano huu utatangaza utalii kwa wageni hao kupata fursa ya kutembelea mbuga ya Serengeti na vivutio mbalimbali vya utaliii hapa nchini