Habari

Imewekwa:: Jun, 16 2020
News Images

Msimu wa ununuzi wa pamba 2020-21 ulizinduliwa rasmi tarehe 15 Juni 2020 katika kijiji cha Mbogwe wilayani Nzega na mkuu wa mkoa wa Tabora Ndg. Aggrey Mwanri. Uzinduzi huo ulitanguliwa na mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania Ndg. Marco Mtunga kutangaza bei elekezi ya pamba kwa msimu wa 2020-21 kuwa ni shilingi 810/= kwa kilogramu moja ya pamba mbegu. Akielezea namna muafaka wa bei hiyo ulifikiwa kwa vikao vilivyotangulia ambapo wadau (wawakilisha wa wakulima na wafanyabiashar/wachambuaji) wlalikaa na kufikia muafaka wa bei hiyo chini ya usimamizi wa serikali. Bei iliyotangazwa ni ndogo kulinganisha na msimu uliotangulia,akielezea kuhusu kushuka kwa bei ya pamba kwa msimu huu Mkurugenzi Mkuu alitaja sababu ya janga la korona limechngia kwa kiwango kikubwa kushuka kwa bei kutokana na mahitaji ya pamba katika viwanda vya nguo kupungua kwa kiwango kikubwa.