Habari

MAADHIMISHO SIKU YA PAMBA DUNIANI YATIMIA MIAKA MITATU
Pamba ni zao la zao kuu la nyuzi ambalo halitokani na kutengenezwa tokea viwandani hivyo kulifanya liwe na upekee wa aina yake na kupewa heshima kutokana na upana wake wa matumizi miongoni mwa mazao ya nyuzi duniani.
Upekee hu wa pamba umeisukuma WTO shirikisho la biashara duniani kutenga siku maalum ya kuadhimisha umuhimu wa zao hili katika maisha ya kila siku ya binadamu, uhitaji wa mazao yatokanayo na nyuzi umekuwa ukiongezeka kutokana na onezeko la idadi ya watu duniani na upendeleo wa watu wengi kuhitaji mavazi yatokanayo na pamba kwa sababu yanawafanya wajisikie vema katika vipindi tofauti vya joto na baridi.
Shirikisho la Biashara la umoja wa mataifa likaitangaza siku ya tarehe 7 Oktoba kuwa siku ya pamba duniani na mwaka huu inatimiza miaka mitatu {3} tangu kuanzishwa kwake,
Pamoja na pamba kuwa zao kuu la nyuzi linalofaa kutumika katika nyakati tofauti katika mavazi pia zao hili limekuwa na matumizi zaidi ya sekta ya mavazi na kutumika pia kuonesha umuhimu katika sekta ya matibabu.
Umuhimu wa zao la pamba umeonekana katika;
- Kuondoa umaskini katika jamii: kutokana na kuwa chanzo cha kuondoa umaskini katika nchi nyingi kutokana na kutoa fursa kuanzia shambani hadi ajira katika maeneo ya viwanda
- Mazao ya pamba yanaoza haraka kulinganisha na mazao yatokanayo na viwanda ivyo kuyafanya yawe miongoni mwa mazao rafiki kwa mazingira
- Ni zao pekee la nyuzi linalotokana na bidhaa za nyuzi na chakula
- Pamba ni mojawapo ya zao linaloweza kuvumilia hali ya upekee ya ukame hivyo kulimwa katika maeneo mengi ambapo mazao mengine hayawezi stawi
- Wadau wa pamba kote duniani uadhimisha siku hii muhimu kuonesha namna ambavyo zao ili linagusa maisha ya kila siku ya watu kuanzia kutoa bidhaa mbalimbali za nyuzi hadi chakula katika mnyororo wake mrefu wa thamani.
- HERI YA SIKU YA PAMBA DUNIANI…………….