Habari
Imewekwa:: Oct, 07 2020

Siku ya pamba duniani huadhimishwa kila Oktoba 7 katika mwaka kwa dhamira ya kutambua pamba kama bidhaa ya ulimwengu na jukumu lake katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi nyingi zinazoendelea na nchi zilizoendelea.
Mwaka 2020 maadhimisho haya yanatimiza mwaka mmoja tangu yalipozinduliwa na shirika la biashara ulimwenguni "WTO" likiwa ni wazo lilitokana na mapendekezo ya nchi nne vinara kwa uzalishaji wa pamba(Cotton - 4: Benin, Burkinafaso, Mali na Chad ) katika bara la Afrika
Siku hii ilianzishwa kwa malengo makuu manne(4)
- 1.Kuwezesha ufikiaji wa taarifa na kujenga ujuzi kwa wadau wote wa pamba katika uzalishaji, mabadiliko ya kisekta na biashara.
- 2.Kushirikisha na kuwaleta pamoja wafadhili na wanufaika ili kuimarisha ufadhili na misaada ya uwekezaji kwa maendeleo ya pamba.
- 3.Kutafuta ushirikiano mpya na sekta binafsi na wawekezaji wa viwanda vinavyohusiana na pamba na uzalishaji katika nchi zinazoendelea
- 4.Kukuza na kupiga hatua zaidi katika matumizi ya teknolojia, utafiti na maendeleo ya pamba.