Habari

Imewekwa:: May, 20 2022
News Images

MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA WAZINDULIWA HUKU BEI IKIPAA KWA 48%

Pamba ni zao la kimkakati nchini lakini vilevile ni zao mama linalowainua kiuchumi wakulima wengi wa kanda ya ziwa, hilo limedhihirishwa wakati wa uzinduzi wa msimu wa ununuzi wa pamba 2022-2023 ambapo bei pamba imetangazwa kuwa TZS 1560 na kupokelewa kwa nderemo na wakulima wengi waliohudhuria sherehe hizo za ufunguzi wa msimu.

Bei yap amba msimu huu imepanda kwa Zaidi ya shilingi 500 ambalo ni ongezeko kubwa katika miaka ya hivi karibuni ikiwa ni sawa na asilimia 48 kulinganisha na bei yam waka uliotangulia ambapo pamba ilinunuliwa kwa shilingi 1050 msimu ulipofunguliwa

Sherehe za ufunguzi wa msimu mwaka huu zimefanyika kitaifa leo Mei 20,2022 katika mkoa wa Mwanza wilaya ya Magu Kijiji cha Mahaha zikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na wananchi toka maeneo mbalimbali

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mgeni Rasmi Mh. Johari Samizi mkuu wa wilaya ya Kwimba ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amesema msimu huu wa kilimo uzalishaji wa pamba unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 40 toka tani 144,000 msimu uliopita hadi kufikia tani 200,000 msimu huu.

Mh.Johari alibainisha kuwa ongezeko ilo ni chini ya matarajio yaliyowekwa kwa Tanzania kuzalisha Zaidi,hali ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na uhaba wa mvua hasa kipindi ambacho wakulima wa pamba walikuwa wakipanda.

Katika kutatua changamoto ya utegemezi wa mvua kwa wakulima ambayo kwa kiasi kikubwa inashusha uzalishaji kwa wakulima mhe. Johari aliwaasa wadau wa pamba kuangalia uwezekeno wa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliajikwa kuanza na mashamba ya mifano.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania akizungumza wakati wa sherehe hizo alitoa rai kwa wakulima kutoa ushirikiano kwa wakulima alisema “wakulima wengi wa pamba mmekuwa mkishindwa kuwapa ushirkiano wakaguzi wa pamba wanapobaini kuwepo kwa pamba chafu katika vituo vya kuuzia pamba kwa kuhofia kutouza pamba yao bila kufahamu kuwa pamba chafu ndio chanzo kikuu kinachofanya bei ya p amba yetu iporomoke katika soko la dunia”

Mkurugenzi Mkuu vilevile aliwaasa wakulima wjiunge katika ushirika ili kuweza kuleta mabadiliko wanayoyataka baada ya kuwa walalamikaji wa uendeshaji unaowanyima manufaa wa vyama vyao vya msingi vya ushirika