Habari

WAKULIMA WA PAMBA KUENDELEA KUSAMBAZIWA VIUATILIFU KWA WAKATI
Wakulima wa zao la pamba kanda ya magharibi wamehahakishiwa kupatiwa huduma bora na za wakati ili waweze kudhibiti wadudu wasiharibu mazao yao na kuwasababishia hasara.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi aliyekuwa akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania wakati akipokea ya shehena viuadudu ekapaki milioni moja na laki nne vitakavyosambazwa kwa wakulima wa pamba kote nchini. Viuadudu hivyo ni muendelezo wa usambazaji wa viuadudu vya kudhibiti wadudu waharibifu wa pamba zoezi lilioanza tangu mwezi Desemba 2021,na linatarajiwa kuendelea hadi kufikia hatua ya kuvuna pamba kwa wakulima.ambaye amewataka wakulima wa pamba kuwa tayari kwa mapambano dhidi ya wadudu waharibifu wa pamba kwa kutumia viuadudu vinavyosambazwa na serikali kupitia Bodi ya Pamba
Mkurugenzi amesema kuwa viuadudu hivyo vimeagizwa kwa kuzingatia hitaji hasa la wakulima kwa kulenga wadudu wanaosumbua wakulima wakulima kwa kiasi kikubwa katika misimu ya karibuni. Aliwataja wadudu hao kuwa ni wale wafyonzao(mfano CHAWAJANI) na watafunao zao la pamba
Bwana Shimbe alieleza kuwa hadi kufikia tarehe 24 Februari jumla ya viuadudu 2.7 milioni ekapaki zilishawafikia wakulima wote wa pamba kanda ya mashariki na kanda ya magaharibi,vilevile hadi kufikia mwisho wa msimu huu wa kilimo jumla ya ekapaki milioni nane (8) za viuaduduvyenye thamani ya takribani milioni 40 vinatarajiwa kusamabzwa kwa wakulima.
katika maelekezo aliyotoa Mkurugenzi wa Huduma za usimamizi alisisitiza kwa watendaji waliokasimiwa jukumu kugawa viuadudu hivyo katika ngazi ya wakulima kuwa waadilifu na kuepuka wizi wa pembejeo hizi muhimu kwa wakulima kujinufaisha binafsi kwani kufanya hivyo ni kuhujumu juhudi ya wakulima na serikali katika kujenga uchumi