Habari

Imewekwa:: Nov, 03 2022
News Images

WAKULIMA WA PAMBA WAITIKIA VIPIMO VIPYA UPANDAJI PAMBA

Uzalishaji wa zao la Pamba Nchini umeongezeka na kuleta tija kwa wakulima baada ya kutumia Vipimo vipya vya upandaji pamba vya sentimeta 60 Kwa 30 ambapo awali walitumia sentimeta 90 kwa 40 kupanda kati ya mstari na mstari na mche na mche

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi huduma za usimamizi kutoka Bodi ya Pamba James Shimbe alipofanya mahojiano ya redio hivi karibuni jijini Mwanza na kueleza kuwa mabadiliko hayo yameongezeka upandaji wa miche kwa ekari Mara mbili kutoka Miche 22,222 Hadi kufikia Miche 44,444 kwa ekari.

Shimbe ameeleza kuwa Mikakati waliyonao ni kuhakikisha wanafikia Tani Mil 1 Kwa mwaka 2025-2026 ili kuwawezesha wakulima kuwa na kilimo Cha kisasa na kitakachokuwa na manufaa kwao.

"Manake ili wakulima wawe na kilimo chenye tija ni lazima kuwapatia majembe ya kupalilia ya kukokotwa na wanyama kazi Kwa mkopo ambapo itarahisisha na Kama mkulima atakuwa amelima Kwa kufuata mistari" Alisema James.

Hata hivyo amesema kuwa katika msimu wa kilimo 2021/22 zaidi ya asilimia 40 ya wakulima wa pamba wamehamasika kulima kwa kutumia vipimo vipya vya upandaji kutokana na balozi wa Pamba Kwa kushirikiana na maafisa kilimokutoa elimu namna ya kulima zao Hilo.

Yasinta Fidelis ni Mtafiti kutoka TARI ameeleza kuwa kiujumla kanuni mpya ya upandaji wa zao la pamba imeleta tija kutokana na teknolojia waliyoipeleka Kwa wakulima.

"Ile ni teknolojia ambayo tulitoa Kwa wenzetu walioendelea katika zao la pamba huko Brazil imeongeza tija kwa wakulima" Alisema Fidelis.

Fidelis ameeleza kuwa kutokana na utafiti walioufanya katika Vipimo mbalimbali na udongo wa aina tofauti na kugundua Vipimo vya sentimeta 60 Kwa 30 ndivyo vinaweza kuleta tija katika uzalishaji wa zao la pamba.

"Tukilinganisha awali na sasa katika Vipimo vya sentimeta 90 kwa 40 utofauti upo Kwa sababu tumeongeza idadi ya mimea kwa ekari katika zao Hilo na kuleta tija.

Richard Jagi ni mkulima wa Pamba kutoka Kasamwa wilaya ya Geita ameeleza kuwa Kwa kutumia Vipimo vipya wameweza kupiga hatua na kuyafikiamafanikio yenye tija kupitia zao la pamba.

"Mfano mzuri ni Mimi mwenyewe msimu huu nililima Kwa kufata vipimo vipya sentimeta 60 Kwa 30 ekari moja nilivuna kilo 1258 kutoka kwenye shambani langu"

Jagi amesema kuwa kipindi Cha nyuma walikuwa wanatumia njia za kienyeji Kwa kutupa mbegu lakini tangu wamepata elimu namna ya kupanda Kwa kufata mistari kulima wameweza kupata faida tofauti na nyuma.

Hata hivyo amesema kuwa mbali na kupata mafanikio elimu bado inahitajika Kwa wakulima ili waweze kulima kilimo chenye tija na kitakachowaletea mafanikio Kwa kutumia Vipimo vipya.