Habari

Imewekwa:: Oct, 06 2022
News Images

MAADHIMISHO YA SIKU YA PAMBA DUNIANI OKTOBA 7

Siku ya Pamba Duniani Ni Nini??

Siku ya Pamba Duniani ni Maadhimisho kuonyesha Pamba kama zao muhimu duniani na Fursa zilizopo kupitia pamba pamoja na mchango wake chanya na wa kudumu kwa jamii mbalimbali. Jumuiya ya kimataifa ikialikwa kuungana na kusherehekea nyuzi hii asilia muhimu zaidi duniani!

Siku ya Pamba Duniani ilianzishwa mnamo mwaka 2019, wakati wazalishaji wakuu wanne wa zao la pamba barani Afrika Benin, Burkina Faso, Chad na Mali walipendekeza kwa Shirika la Biashara Duniani (WTO) mnamo Oktoba 7 kila mwaka kuwa maadhimisho ya Siku ya Pamba Duniani

Katika miaka mitatu (2) mfululizo kuanzia mwaka 2019, siku ya tarehe 7 Oktoba ilitoa fursa ya kushiriki maarifa na kuonyesha shughuli mbalimbali zinazohusiana na pamba.

Kwa kuwa Umoja wa Mataifa umeidhinisha rasmi Siku hii ya Pamba Duniani, fursa hii adhimu inajenga ufahamu wa haja ya upatikanaji wa soko la pamba na bidhaa zinazohusiana na pamba kutoka nchi zenye maendeleo duni, inakuza sera endelevu za biashara na kuziwezesha nchi zinazoendelea kunufaika zaidi na kila hatua. ya mnyororo wa thamani wa pamba

Jambo Gani Kuu ufanyika siku ya Pamba Duniani?

Wadau kutoka jumuiya ya kimataifa ya pamba wanakusanyika ili kuzungumza juu ya faida nyingi za pamba kutoka kwa sifa zake kama nyuzi asilia, hadi faida nyingi ambazo watu hupata kutokana na uzalishaji wake. Mada mwaka huu ni pamoja na

Kwa nini Siku ya Pamba Duniani ni Muhimu?

Kwa sababu pamba ni zao la nyuzi asilia lenye upekee usiofanana na nyuzi nyingine ya asili.

  • Ni zao linalopunguza umaskini katika baadhi ya nchi zilizoendelea duniani, na linatoa ajira endelevu na zenye staha kwa watu kote ulimwenguni kuanzia kilimo usokotaji wa nyuzi na ufumaji wa nguo.
  • Nyuzi ya Pamba Inaharibika haraka baanda ya matumizi (kama nguo au kitambaa) ikilinganishwa na nyuzi mbadala, hivyo kupunguza kiwango cha plastiki zinazoingia kwenye njia zetu za maji na kusaidia kuweka mazingira yetu salama
  • Ni bidhaa pekee ya kilimo ambayo hutoa nyuzi na chakula.
  • Pamba ni zao linalovumilia ukame na hustawi katika maeneo ambayo hakuna mazao mengine yanaweza stawi.

MADA MWAKA HUU

“Uendelevu, Ushiriki wanawake katika pamba, ushirikiano wa chapa za nguo na wauzaji rejareja “

#pamba #dhahabunyeupe