Leseni ya kununua pamba mbegu
Leseni ya kununua pamba mbegu
Imewekwa: 26 February, 2026
Mdau wa pamba anayehitaji kuingia katika biashara ya kununua na kuchambua pamba mbegu anapaswa kuwa na vielelezo vifuatavyo ili aweze kupata leseni ya kununua pamba mbegu
- Leseni ya mfanyabiashara
- Udhibitisho wa uanachama wa chama cha wafanyabiashara wa pamba (TCA)
- Kibali kutoka halmashauri ya wilaya husika
- Udhibitisho wa kumiliki au kukodi kiwanda cha kuchambua pamba mbegu
Maombi yote yawasilishwe Bodi ya Pamba Tanzania kupitia mfumo wa mtandaoni kwa tovuti ya
https://ekilimo.kilimo.go.tz/