Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bodi ya Pamba Tanzania

TCB YALENGA KUONGEZA UBORA WA PAMBA KWA ASILIMIA 75 KUPITIA UIMARISHAJI WA PROGRAMU ZA MAFUNZO

Imewekwa: 21 May, 2026
TCB YALENGA KUONGEZA UBORA WA PAMBA KWA ASILIMIA 75 KUPITIA UIMARISHAJI WA PROGRAMU ZA MAFUNZO

Bodi ya Pamba Tanzania imetoa Semina elekezi kwa Maafisa Kilimo wa Serikali, Maafisa Ugani kupitia Mpango a wa Jenga Kesho Bora (BBT) na Viongozi wa Amcos juu ya Ubora na Usafi wa Pamba kuelekea msimu wa Ununuzi wa pamba 2026/2027.

Aidha, Viongozi wa Amcos pamoja na BBT wametakiwa kuendelea kuwaelimisha wakulima ili wasiuze Pamba chafu kwani Pamba inauzwa na kununuliwa kwa sifa ya ubora na wingi na ikiuzwa na ubora hafifu haiwezi kushindana ipasavyo kwenye soko la dunia na kupata bei nzuri

‎Akitoa elimu ya Ubora na Usafi wa Pamba, wakati wa semina elekezi iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri wilayani humo,  Afisa Kilimo Mwandamizi wa Bodi ya Pamba kutoka kitengo cha Maabara ya Usanifu wa madaraja ya Pamba, Bi. Sharifa Salum alisema kuwa kwenye soko la Dunia kuna ushindani wa ubora wa Pamba na kwamba pamba safi ni ile ambayo haina uchafu, njano wala makokwa.

‎Amesema asilimia 65 ya wakulima wa Kanda ya Magharibi wanategema Pamba kama zao kuu la Biashara na pia ni moja ya mazao ya Kimkakati anayochangia pato la Taifa kwa asilimia 3, na kuchochea ukuaji wa Maendeleo katika jamii.

‎"Pamba ikichanua ivunwe kwa wakati, asilimia 60 ya ubora wa Pamba ni mbegu na asilimia 40 ni nyuzi...jukumu letu ni kwenda kufanya hamasa ili wakulima wasipoteze ubora wa pamba, tuelewe kuwa unyevu wa asili wa Pamba ni asilimia 8, ikizidi hapo Pamba hiyo itakuwa imechanganywa na Maji" amesema Sharifa.

‎Alisema Wajibu wa kitengo cha Usafi na Ubora wa Pamba katika Maabara Kanda ya Shinyanga ni kuainisha viwango vya ubora na kutoa Cheti cha ubora ili kujitangaza Pamba duniani na chet hicho hutumika kusafirishia marobota kwenda nchi mbalimbali zinazonunua Pamba ya Tanzania.

‎Ameongeza kuwa Pamba inayotarajiwa kuuzwa kwenye soko la Dunia takwimu za ubora ziko chini katika msimu miwili ya 2024/25 ambapo viwango vya ubora vilishuka mpaka kufikia asilimia 7 na msimu uliofuta viwango vya ubora vilipanda na kufikia asilimia 21 ambapo kupitia Balozi wa Pamba na Maafisa Ugani wa BBT walitoa Elimu kwa wakulima wa Pamba.

‎"Lengo ni kufikia asilima 75 ya ubora wa pamba, msimu huu 2026/2027 kabla ununuzi wa Pamba hatujaanza tuongee na Maafisa Kilimo wa BBT, viongozi wa Amcos ambao wananunua Pamba na kusimamia ubora ili tutoke kwenye asilimia 21 . Sheria iko wazi kwa wanaochafua Pamba na atakayekuwa mkaidi tutamkabidhi kwenye vyombo vya kisheria" amesema.

‎Awali akifungua semina hiyo, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wilaya hiyo, Thomas Masanja Shilabu amewataka viongozi wa Amcos kutopokea Pamba chafu, pia wazingatia Usafi wa maghala ikiwemo kupulizia maghala na kwamba wamepitisha kwenye Mwongozo ili wakasimamie wajibu wao.

‎"Tukiuza Pamba ni maandalizi ya msimu ujao, pia tukaanze kusajili wakulima, Afisa ugani ukikuta wakulima wanauza Pamba wasajili hapohapo ili kurahisisha zoezi la usajili...karani akihujumu Pamba, mkataba wake utasitishwa mara moja na ikitokea uchakachuaji wa mzani, karani au kiongozi wa Amcos atachukuliwa hatua kwa mujibu wa mikataba yao na tuhakikishe Pamba inayonunuliwa inakuwa na ubora" alisema.

‎Afisa Kilimo kupitia Mpango wa Jenga Kesho Bora (BBT) kutoka kijiji cha Mwangudo, Sara Ngairo, amesema kupitia mafunzo hayo atahakikisha anasimamia zao la pamba, kuelimisha wakulima kuchambua na kuikausha kabla ya kuuzwa ghalani na pia Mafunzo hayo yatawaongezea Ushirikiano baina yao na viongozi wa Amcos na Maafisa Ugani wa serikali ili washirikiane kumwelimisha mkulima auze Pamba safi.

 

slot gacor