Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bodi ya Pamba Tanzania

MHE. CHONGOLO: UHAKIKA WA PEMBEJEO, MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KULETA TIJA YA ZAO LA PAMBA

Imewekwa: 19 April, 2026
MHE. CHONGOLO: UHAKIKA WA PEMBEJEO, MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KULETA TIJA YA ZAO LA PAMBA

Waziri wa Kilimo Mhe.Daniel Chongolo amesema serikali imeboresha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo kwa kuhakikisha zinawafikia wakulima kwa wakati na kwa gharama nafuu.
 Ameongeza kuwa juhudi hizo ni sehemu ya mkakati mpana wa serikali wa kuimarisha sekta ya kilimo na kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa.

Chongolo ameyasema hayo katika mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Pamba uliofanyika tarehe 16 Aprili katika ukumbi wa Jakaya kikwete jijini Dodoma huku kauli mbiu ya mkutano huo ikiwa ni "Nguvu ya pamoja kwa Tasnia ya Pamba Endelevu"

Aidha amesema Sera ya kilimo ya mwaka 2023 inaeleza kwamba kila kijiji kinatakiwa kuwa na Afisa ugani mmoja ambapo Dhamira ya Serikali ni kukuza uchumi wa mkulima kufikia 2030.
Ameeleza kuwa wakulima wengi wa pamba bado wanatumia mbinu za zamani za kilimo, hali inayochangia kushuka kwa tija licha ya baadhi yao kuwa na mashamba makubwa.

Kutokana na changamoto hiyo, serikali imeendelea kuweka mikakati bora ya kuwahamasisha wakulima kutumia teknolojia za kisasa ili kuongeza uzalishaji.
 Sanjari na hayo serikali imeongeza Jitihada Kukuza Uzalishaji wa Pamba huku ikiendelea kuwekeza nguvu kubwa katika sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na kuinua uchumi wa wakulima pamoja na wananchi kwa ujumla,
Chongolo amesisitiza kuwa mkutano huo ni muhimu katika kujadili mikakati madhubuti ya kuendeleza sekta ya pamba, ambayo ni miongoni mwa mazao muhimu ya biashara nchini.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ameishukuru Bodi ya Pamba kwa kuweza kuchagua mkoa huo kufanya mkutano wao akiongeza kuwa "kama mkoa tumejipanga kuhakikisha tunasapoti juhudi za Serikali katika Wizara ya Kilimo"
 

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), Christopher Gachuma akichangia katika mkutano huo, amekiri kuwa changamoto ya bei ndogo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na kutegemea soko la kimataifa. Wakati bei ya dunia inaposhuka, mkulima wa ndani anajikuta katika wakati mgumu.

Ili kukabiliana na hali hii, Gachuma ameshauri serikali na sekta binafsi kuwekeza zaidi katika viwanda vya ndani. “Tukichakata pamba yetu wenyewe, tutatengeneza soko la uhakika la ndani ambalo halitayumbishwa na bei za New York au Liverpool,” amesema Gachuma. Hii itasaidia kuhakikisha kuwa zao la pamba

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Bw. Marco Mtunga, amesema kuwa zao hilo ni la kimkakati kwa uchumi wa nchi na limelengwa kuongeza uzalishaji hadi kufikia tani milioni 1 ifikapo mwaka 2030. Ameeleza kuwa Bodi ya Pamba imeratibu utoaji wa huduma za Ugani kupitia programu ya BBT-Ugani pamba ambapo  zaidi ya maafisa ugani 700 wameajiriwa katika mpango huo na kuwezesha kuongeza wigo wa uzalishaji wa pamba kutoka tani 149,000 msimu wa 2024/2025 hadi kufikia tani 222,000 msimu wa 2025/2026 na msimu huu wa 2026/2027 uzalishaji wa pamba unatarajiwa kuongezeka hadi kufikia tani 300,000

Kwa upande wa wakulima ambao ni moja ya wadau muhimu walioshiriki mkutano huo maalum, wameiomba Serikali kuendelea kusogeza huduma za ugani karibu na mmoja wa wakulima waliowasilisha maoni yao Bw. Walwa Malimi kutoka Chato alieleza namna alivyaonza na kilimo cha kuvuna kilo 200 za Pamba kwa ekari; ambapo baada ya kuimarishwa kwa huduma za ugani amefanikiwa kuzalishaji wa kilo 2,000 kwa ekari moja.

Washiriki kwenye Mkutano ni pamoja na Mhe. David Silinde (Mb), Naibu Waziri wa Kilimo; Bw. Gerald Mweli, Katibu wa Mkuu wa Wizara ya Kilimo; Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo; Wakulima; Wabunge na Wakuu wa Mikoa inayolima zao la Pamba; Wanaushirika; Wafanyabiashara; na Wawekezaji.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 



Serikali itaendeleza jitihada za kuimarisha zao la Pamba kwa kutoa elimu na pembejeo kwa wakulima ili kuleta tija na bei yenye uhalisia kwa manufaa yao na wadau wa mnyororo mzima wa zao hilo.

Amesema Mhe. Daniel Chongolo (Mb), Waziri wa Kilimo wakati wa Mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Pamba tarehe 16 Aprili 2026, Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Bw. Marco Mtunga, amesema kuwa zao hilo ni la kimkakati kwa uchumi wa nchi na limelengwa kuongeza uzalishaji hadi kufikia tani milioni 1 ifikapo mwaka 2030. Ameeleza kuwa Bodi ya Pamba imeratihu utoaji wa huduma za Ugani kupitia programu ya BBT-Ugani Pamba ambayo imewezesha kuongeza wigo wa uzalishaji wa zao hilo ambapo katika ~mwaka~ msimu huu wa ~mwaka~kilimo wa 2025/2026 tani laki 3 zinatarajiwa kuzalishwa.

Maoni mbalimbali yaliyotolewa yamejikita katika kuiomba Serikali kufanya tathmini za kina kuhusu bei ya Pamba ili imnufaishe mkulima; kuleta teknolojia za kısasa za kilimo zitakazoongeza uzalishaji wenye tija; ruzuku za viuadudu na pembejeo.

Kwa upande wa wakulima, wameiomba Serikali kuendelea kusogeza huduma za ugani karibu na wakulima na mmoja wao akieleza kuwa alianza na kilimo cha ekari moja wilayani Chato na kuvuna kilo 200 za Pamba; ambapo baada ya kuimarishwa kwa huduma za ugani amefikia uzalishaji wa kilo 2,000 kwenye hiyo ekari moja.

Washiriki kwenye Mkutano ni pamoja na Mhe. David Silinde (Mb), Naibu Waziri wa Kilimo; Bw. Gerald Mweli, Katibu wa Mkuu wa Wizara ya Kilimo; Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo; Wakulima; Wabunge na Wakuu wa Mikoa inayolima zao la Pamba; Wanaushirika; Wafanyabiashara; na Wawekezaji.