Omba Leseni: Kuchambua Pamba

Omba Leseni: Kuchambua Pamba
  1. Mwombaji wa Leseni lazima awe na kiwanda chake mwenyewe au cha kukodi.
  2. Kiwanda kinachoombewa Leseni lazima kiwe kimekaguliwa na kupasishwa na Mkaguzi wa Viwanda kutoka Bodi ya Pamba
  3. Mwombaji wa Leseni lazima awe Mwanachama wa Mamlaka ya Pamba Tanzania (TCA).
  4. Mwombaji wa Leseni ana wajibu wa kumtaarifu Mkaguzi wa Viwanda wa Bodi ya Pamba kuhusu uhitaji wa ukaguzi wa kiwanda husika.
  5. Mwombaji wa Lesni lazima azingatie sheria, kanuni na taratibu zingine zote zinazosimamia uendeshaji wa kiwanda.