Jenga au Panua: Kiwanda cha kuchambua Pamba

Jenga au Panua: Kiwanda cha kuchambua Pamba

Mtu au Kampuni yenye nia ya kujenga au kupanua kiwanda cha kuchambua pamba itaruhusiwa kufanya hivyo baada ya kuwasilisha Bodi ya Pamba Tanzania taarifa zifutazo na kuidhinishwa;

  • Mwombaji kibali cha kupanua kiwanda lazima awe ni mmiliki wa kiwanda husika
  • Upanuzi wa kiwanda lazima ukaguliwe na kupasishwa na Mkaguzi wa Viwanda wa Bodi ya Pamba kabla na baada ya kukamilika.
  • Mwombaji wa kibali asiwe na mgogoro wa kibiashara na kampuni ya nje au ndani ya nchi
  • Ni wajibu wa mwenye kiwanda kuonesha nia ya kiwanda chake kukaguliwa na kupasishwa kabla ya kupatiwa kibali kwa ajili ya uchambuaji wa pamba.