Pata Kibali: Kusafirisha Pamba Nje ya Nchi

Pata Kibali: Kusafirisha Pamba Nje ya Nchi
  • Mwombaji wa Kibali cha Kusafirisha robota nje ya nchi lazima awe na Leseni ya Biashara, uthibitisho wa uwakala wa mnunuzi wa Pamba mbegu
  • Mwombaji wa Kibali lazima awe na Leseni ya kuuza Pamba nje ya nchi
  • Mwombaji lazima arejeshe nakala ya Kibali anachopatiwa ndani ya siku kumi na nne (14) kabla ya kupatiwa kibali kipya
  • Mwombaji wa kibali hatauza Pamba kwa kubadilishana na kitu kingine
  • Mwombaji wa kibali ambaye ni wakala wa usafirishaji lazima aonyeshe namba ya Leseni ya mwenye Pamba anayemwombea Kibali
  • Mwombaji lazima awe na cheti cha ubora wa Pamba anayotaka kuuza nje ya nchi.
  • Mwombaji wa kibali lazima awe amesajiri mikataba yake ya kuuza Pamba na makampuni ya nje.